BI HARUSI AFARIKI BAADA YA SIKU MOJA KUFUNGA NDOA (SEHEMU YA PILI)

Ilipoishia...........
                 Mama wa bwana harusi aliporudi jikoni mama yangu akaanza kumsimulia yalokuwa                            yamemkuta huko nje, yule mama alimwambia mama yangu "mie niliacha kupika baada ya                  kuona mtu huyo akibeba sufuria" na akaongezea kusema kuwa mtu huyo "alimfahamu                         kwani alikufa zamani na aliacha mke na mtoto mmoja", kwa hiyo ulikuwa msikule.


Sasa endelea.....................
                    Muda kidogo mvua ilikata na watu wote tukarudi ukumbini ya kafanyika yote yaliyopaswa na hapo muda wa Bi harusi na Biharusi kuingia ukumbini ukawadia, maharusi wakaingia ukumbini na watu wakapigia vigelegele, vifijo na ndelemo. Baada wakakaribishwa viti vyao ili wapate kutulia na harusi kuendelea.

Harusi iliendelea vizuri na muda ukafika muda wa kutoa zawadi, alianza kutoa Baba wa Bwana Harusi kisha akafatia mama mtu, alinyanyuka na kutoa zawadi alimzawadia ng'ombe baaada ya kutoa zawadi hiyo, alikuwa na haya ya kusema "Mwanangu Shamimu 'ambaye ndo Bi Harusi' umekuja kwenye familia yangu napenda nikukaribishe sana tena sana ila nakuomba uje kuijenga familia na usije kuivunja familia"!!!! "na pia msituharibie urafiki wangu" mwisho wa neno la mzazi, kila mtu akashangaa kusikia maneno hayo lakini walikaa kimya kwani zilikuwa familia mbili ambazo zilikuwa zinafahamiana.

Basi zawadi ziliendelea na kila mtu akatoa zawadi aliyokuwa nayo. Mida ya saa 12 Alasiri ndipo Maharusi waliruhusiwa kuingia ndani maana hapo ndo ulikuwa mwisho wa sherehe hiyo. Bi Harusi alitangulia mbele na Bwana Harusi akawa nyuma, ambavyo si taratibu za kimila. Tukio hili lililotokea bado lilizidi kuwachanganya sana watu maana hapo yamekuwa matukio mengi sana ukijumlisha na yaliyotokea nyumbani kwao na Bi Harusi.

Maharusi wakaingia ndani lakini kabla hawajaingia ndani Bi harusi aligoma kuingia chumbani, bahati nzuri alikuwa na Shangazi yake, shangazi alipomuuliza kuna kitu gani bi harusi akamjibu "Shangazi kwani aliyekaa kitandani wewe humuoni!!!!?, maana aliyekaa kitandani ni mtu tofauti na mume wangu" shangazi hakujali akambembeleza ili apate kuingia chumbani kwani shangazi yake alifikiri ni wasiwasi wake tu. Bi Harusi akakubali akaingia chumbani na wakafanya taratibu zote zilizokuwa zikitakikana, walipomaliza kila mtu akaondoka kwao.

Ikumbukwe sherehe hizi zilifanyika siku mbili yaani Jumamosi kwao na Bi Harusi na Jumapili kwako na Bwana Harusi. Sasa kesho yake ambayo ni Jumatatu kuliwa na arobaini ya msiba katika kijiji cha pili kutoka kijijini hapo palipokuwa na sherehe. Hata hiyo nayo nilikuwepo, sasa mida ya saa 7 mchana mara tukamuona mmama mmoja analia lakini baada ya kumuangalia tu tukakumbuka kuwa tulimuona kwenye sherehe, ikabidi tumuulize nini kimejiri akatuambia ya kuwa "Bi Harusi tuliyemfanyia harusi jana amekufa.

Itaendelea................................
Share on Google Plus

About NASWIHEART

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni