BI HARUSI AFARIKI BAADA YA SIKU MOJA KUFUNGA NDOA

KISA HIKI KINANISIKITISHA MNO KILICHOTOKEA MKOANI KAGERA
Mnamo mwaka 2011 kulitokea kitu ambacho sitakisahau katika maisha yangu yote. Siku moja kulitokea sherehe kubwa katika kijiji cha Kasharu Wilayani Bukoba Vijijini Mkoani Kagera, nyumbani kwa Mzee Qassim, sherehe hiyo ilikuwa ni wapendanao wawili yaani walikuwa wanafunga ndoa. 

Maharusi hao walikuwa ni wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM). Walipanga harusi iwe ni wakati wa likizo yaani watakapopata likizo ndo waweze kufuga ndoa, na kweli mungu aliwajaalia wakaifikia siku hiyo lakini siku hiyo haikuwa ya furaha kwa Bi Harusi kwani alihisi kitu kichwani mwake. Kwa kawaida katika kabila la Wahaya, mwali ukiwa ndani huruhusiwi kutoka nje kwa siku kadhaa mpaka pale utakapotoka unaenda kwa mume wako. Lakini kwa Bi Harusi huyo haikuwa hivyo.

Siku tuliletewa kadi ya mwaliko na watu wakaitika kuhudhuria ndoa na watoto wao, marafiki zao, jamaa zao na wengine wengi. Sie tulifika saa nne na nusu asubuhi tukawa tumekaribishwa ndani, mara tumekaa tukamuona Bi Harusi anatoka chumbani huku analia kiukweli kila mtu alistaajabu kwani si katika utamaduni wa wahaya. Akapita taratibu akaenda jikoni walikokuwa wakipikia wapishi akamuita mdogo wake na kumkumbatia huku akimuambia maneno haya "KWA HERI MDOGO WANGU SIKU ALEO DO YA MWISHO HUTOWEZA KUNION TENA" akawa aanayarudia maneno haya akimuambia mdogo wake kiukweli kila mtu alishangaa kuona Bi Harusi anaongea maneno kama yale.

Alipomaliza akarudi chumbani, basi na hapo muda uliwadia na sherehe ikaanza, na ikaendelea tu vizuri lakini ulipowadia muda wa kutoa zawadi alianza Baba wa Bi Harusi akasimama kutoa neno kama Baba akaongea vizuri, kitendo hicho kiliwashangaza watu wengi sana kwani baba huyo alikuwa hawezi kuongea tangu mke wake alipopata Udiwani sasa wakajiuliza amewezaje kuongea? kweli swali hilo lilijenga fikra mbaya kichwani mwa kila mtu, kabla watu hawajamaliza kutafakari tukio hilo Baba wa Bi Harusi akatoa zawadi akamaliza lakini cha kustaajabisha zaidi ni kwamba baba alipomaliza tu kutoa zawadi, baba huyo hakuweza kuongea tena mpaka wa leo naandika kisa hiki. Basi harusi iliendelea mpaka saa kumi na mbili jioni na kila mtu akieleke nyumbani kwake na wengine waliendelea kubaki pale hasa vijana wakisubiri kucheza mziki.

Siku ya pili yake ikafika ya Bibi Harusi kwenda kwa mumew, wengine walitangulia kwa kuwa kulikuwa karibu na wengine walibaki kwa ajili ya kuja na Bi Harusi. Nasi tulifika mida ya saa 5:00 asubuhi na tulikaribshwa ukumbini. Muda kidogo mawingu yalitanda na mvua pia ikaanza kunyesha, tulikaribishwa ndani, sasa mimi nilikaa karibu na mlango wa kati, wakati mvua inaendela kunyesha mama yangu akatoka nje kwa ajili ya aja ndogo, akatoka nje anakaa ili aweze ku..... na kabla haja.... ghafla akamuona mtu amevaa mavazi meusi, nywele ndefu, na kucha ndefu na ghafla giza likaanza kutanda mama yangu akakimbia na kurudi ndani na kasimulia kilichomkuta.

Kama dakika tano hivi mie nikaijiwa na hisia akili zangu zikawa zinanituma niangalie juu ya mlango, nilipoangalia hapo nikaona vitu fulani vimefungwa kwenye kitambaa cheusi na kimezungushiwa na hirizi wakati nataka kumuonyesha mama kumbe tayari kuna mwalimu wetu mmoja alikuwa naye tayari kaona sasa sote kwa pamoja tunataka kumuonyesha mama ghafla alitokea mama yake na Bwana Harusi alikuw\ amejifunga kanga moja na huku maziwa yakiwa yapo nje yananing'inia alipoulizwa alidai kwamba ni mihangaiko. Aliporudi jikoni mama yangu akaanza kumsimulia yalokuwa yamemkuta huko nje, yule mama alimwambia mama mie niliacha kupika baada ya kuona mtu huyo akibeba sufuria na akaongezea kusema kuwa mtu huyo alimfahamu kwani alikufa zamani na aliacha mke na mtoto mmoja, kwa hiyo ulikuwa msikule.

TO BE CONTINUED..........................
Share on Google Plus

About NASWIHEART

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni