VITU VINAVYOHITAJIKA
1. Nyanya
2. Vitunguu
3. Karoti
4. Hoho
5. Nyama/Samaki
6. Nyanya chungu kama utakuwa mtumiaji
7. Maharage
8. Mafuta ya kula au mafuta ya mawese itapendeza zaidi ukiwa na Samli
JINSI YA KUANDAA
HATUA YA KWANZA: Koka jiko, chambua maharage, yaoshe vizuri yatie kwenye sufuria, osha nyama yako changanya ma maharage kisha bandika jikoni. Maharage ya kupika kwenye ndizi hayapaswi kuiva sana hivyo yabidi yawe saizi ya kati yasiive sana wala yasibaki mabichi sana.
HATUA YA PILI
Andaa ndizi zako zimenye, baada ya kumaliza kumenya unaangalia maendeleo ya maharage ukikuta yameishakuwa tayari, ipua maharage, tenga sufuria lako la kupikia weka maharage kidogo kisha fuatisha ndizi sufuria likifika katikati weka maharage yalobakia, mboga labda samaki, nyanya chungu, weka viungo vyote isipokuwa ukitumia samli na chumvi hiyo inawekwa baada ya ndizi zako kuchemka yaani zikikaribia kuiva ndo watia hiyo samli.
Kikishaiva unachukua kijiko cha chai unaweka samli kulingana na wingi wa ndizi zako, baada ya dakika 5 unaweka chumvi nayo wasubiri baada ya dakikia 5 kitakuwa tayari kimeiva na kipo tayari kwa kuliwa hivyo waipua unaacha kinapoa kidogo baada ya dakika 5 au 7 unapakua chakula chako unaenjoy na ndizi Bukoba.
KARIBU KWA MAONI, MASWALI HATA KWA KUJUA ZAIDI
![]() |
NDIZI NYAMA |
![]() |
NDIZI NYAMA |
0 maoni:
Chapisha Maoni