Jaji Mkuu Aionya Serikali

Jaji Mkuu Aionya Serikali


Jaji Mkuu nchini Kenya David Maraga, ameilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kufanya maamuzi kinyume cha Sheria na Katiba ya nchi hiyo katika kukabiliana na upinzani.


 Jaji Maraga ametoa kauli hiyo ikiwa imepita masaa kadhaa tokea kufukuzwa kwa mwanasheria maarufu ambaye alikuwa miongoni mwa watu walioshuhudia kuapishwa Raila Odinga katika uwanja wa ‘Uhuru Park’ kufukuzwa nchini humo na kupelekwa Canada.


Katika ukurasa wake wa Twitter Jaji Maraga amesema malalamiko yaliyopelekwa Mahakamani yalikuwa wazi na majukumu ya kufanyia maamuzi yalikuwa ya Mahakama kutokana na kwamba ndio chombo pekee cha kutetea haki kwa kila mmoja pamoja na serikali yenyewe.


Jaji huyo ametoa tamko hilo la kuionya serikali kwa kushindwa kutii sheria kutokana na kitendo cha serikali ya Kenya kuonekana kudharau maamuzi ya mahakama
Share on Google Plus

About NASWIHEART

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni