JESHI la Polisi kanda Maalumya Dar es Salaam limekamata silaha
mbalimbali zikiwemo bunduki, bastola na vifaa vingine vya kufanyia
matukio ya uhalifu pamoja na watuhumiwa mbalimbali wa makosa ya uhalifu
ambao walikuwa wakijiandaa kutekeleleza matukio hayo.
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake leo, Kamanda wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar, Lazaro Mambosasaamesema jeshi hilo limekamata silaha aina
ya AK 47 na watuhumiwa wawili nyumbani kwa mzee Said Omary (62) baada
ya kupata taarifa kuwa kuna wahalifu wanataka kufanya tukio la wizi wa
kutumia silaha.
Aidha Polisi imewakamata watuhumiwa 2 wa wizi wa magari ambao baada ya
kufanyiwa upekuzi walikutwa na radio call, kadi 10 za benki mbalimbali,
leseni za udereva, master keys 15 ambapo baada ya kuhojiwa walikiri
kutekeleza matukio mbalimbali ua uhalifu huku wakionesha magari mawili
na pikipiki moja vinavyodhaniwa kuwa ni vya wizi.
- Blogger Comment
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 maoni:
Chapisha Maoni