Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni Dar es Salaam, Maulid Mtulia kupitia Chama cha CUF na baadaye kujiuzulu nafasi hiyo na kuhamia CCM leo Januari 17, 2018 amechukua fomu ya kuwania Ubunge katika jimbo la Kinondoni kupitia CCM
Mtulia
akiongea mbele ya waandishi wa habari leo amewaomba wananchi wa jimbo
hilo la Kinondoni kuwa subira na kudai ikifika wakati wa kampeni atakuwa
na mambo mengi ya kuzungumza na wao.
"Nawaambia
wana Kinondoni wavute subira mpaka wakati wa kampeni ukianza nitakuwa
na mambo mengi ya kusema nao lakini kwa kipindi hiki wawe watulivu kwa
ajili ya kuzipokea kampeni zetu lakini vile vile kwa ajili ya kufanya
maamuzi" alisema Mtulia
Aliyewahi
kuwa Mbunge wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, Maulid Mtulia kwa tiketi
ya (CUF) Disemba 2, 2017 alitangaza kujiuzulu Ubunge na kujivua
uanachama wa Chama cha Wananchi CUF na kuhamia CCM kwa kile alichodai
anaunga utendaji kazi wa Rais John Pombe Magufuli na serikali ya awamu
ya tano.
Like kwa sana comment pamoja na kushare
0 maoni:
Chapisha Maoni